Mayele: Nitawafunga Kagera Sugar

STRAIKA wa Yanga, Fiston Mayele, amesema kuwa ana shauku kubwa ya kufunga bao lake la kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara na kwa tizi alilopiga, anaamini atafanya hivyo leo dhidi ya Kagera Sugar.

Mayele amefunguka kuwa kufunga kwake bao dhidi ya Simba kutafungua njia zaidi kwake ya kufunga kwenye mechi nyingine zinazokuja mbeleni.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mayele alisema anajua kuwa, ligi ya Tanzania siyo rahisi kutokana na maandalizi ambayo yamefanyika msimu huu, lakini kwake haiwezi kuwa kikwazo kwa sababu kazi yake ni kufunga mabao.

“Natamani kufunga goli kwenye mechi ya kwanza nikiwa na Yanga kwenye ligi ya Tanzania, nimefanya mazoezi ya kutosha, najua nitafunga mbele ya Kagera ingawa siyo rahisi sana kutokana na ugumu wa ligi yenyewe.”

Yanga wanatarajia kushuka dimbani leo Jumatano kwenye Uwanja wa Kaitaba kucheza na Kagera Sugar ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam


Toa comment