Mayele: Nitawafunga KMC Majimaji

STRAIKA wa Yanga Fiston Mayele amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo dhidi ya KMC ambao utapigwa kesho katika uwanja wa Majimaji, Songea.

Mayele alisema yeye atachangia kwa asilimia kubwa ushindi huo kwa sababu malengo yake ni kuendeleza kufunga mabao kwenye mchezo huo.

Mayele amesema timu imepata muda wa kutosha wa kufanya maandalizi na wachezaji wote wako tayari kwa ajili ya mchezo huo na watashirikiana kuhakikisha wanavuna ushindi kwenye mchezo huo.

Akizungumza na Championi Jumatatu Mayele alisema: “Tumejiandaa vizuri, tumepata muda wa kutosha kufanya maandalizi, lengo letu ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo.

“Mimi kama kawaida yangu nikishirikiana na wenzangu nitahakikisha nachangia kupatikana kwa ushindi huo kwa asilimia kubwa kwa sababu nitaendeleza moto wa kufunga.”

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam2179
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment