Mayele: Simba Wajiandae Mwanza, Awahakikishia Yanga Makombe Yote -Video

Fiston Kalala Mayele.

 

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele, baada ya kupita mechi nne mfululizo za Ligi Kuu Bara bila ya kufunga, juzi Ijumaa alivunja mwiko huo wakati Yanga ikishinda 4-0 dhidi ya Mbeya Kwanza, Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Baada ya mchezo huo, Mayele alisema: “Nilijua tu kama nitafunga, sasa nitafunga mechi zijazo zote, walio mbele wajiandae.”

 

Mayele hilo likiwa bao lake la 13 katika Ligi Kuu Bara msimu huu, anaongoza kwa ufungaji sawa na George Mpole wa Geita Gold.

 

Raia huyo wa DR Congo, wikiendi ijayo atakuwa akiiongoza Yanga kucheza dhidi ya Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

 

Kabla ya kucheza na Simba, kesho Jumatatu, Yanga inatarajiwa kumenyana na Biashara United uwanjani hapo ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mayele alisema: “Wakati naingia katika mechi (dhidi ya Mbeya Kwanza), nilikuwa nafahamu kuwa nakwenda kufunga bao, nashukuru Mungu imetokea.

 

“Mimi kutokufunga muda mrefu lilikuwa ni suala la muda tu, naamini kwa sasa kila kitu kipo sawa baada ya kufunga.

 

“Kwa sasa najipanga kuendelea kufunga katika michezo ijayo mfululizo ikiwemo wa FA dhidi ya Simba ili kuipa Yanga mafanikio.

 

“Tuna michezo migumu ijayo na naamini nitaisaidia timu kwa kuhakikisha nafunga. Kama vile nilianza msimu na ubingwa, basi namalizia tena na ubingwa,” alisema Mayele.

 

Mayele ukiwa ni msimu wake wa kwanza kucheza soka Tanzania, tayari amekutana na Simba mara mbili katika Ligi Kuu Bara ambapo alishindwa kufunga, huku akifunga mara moja kwenye Ngao ya Jamii. Hii itakuwa ni mara nne kukutana nao msimu huu.

MAYELE ALICHOJIBU BAADA KUULIZWA KUHUSU MECHI “YANGA BINGWA”3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment