testiingg
The House of Favourite Newspapers

Mayele: Wengine Walisema Mwezi Mzima Sita Tetema, Nilimisi Sana

0
Mshambuliaji wa Yanga Fiston mayele akishangilia bao lake la kwanza katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars

MSHAMBULIAJI hatar wa klabu ya Yanga raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo Fistob Mayele amesema kuwa alimisi sana kutetema kutokana na kuwa na ukame wa mabao katika michezo mitano mfululizo ya mashindano akiwa ndani ya klabu yake ya Yanga.

 

Mayele alifanikiwa kufunga jumla ya mabao matatu (Hat Trick) katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars wakati klabu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 na kurejea katika kilele cha msiamo wa Ligi Kuu ya NBC.

 

“Goli la kwanza lilikuwa la mtoto wangu kwa sababu nimepata mtoto mpya ndo maana uliona mechi ya Zalan nikafunga nikaweka mpira humu aaah nilimisi sana mechi tano kuna wengine walisema mwezi mzima sitatetema, leo namshukuru mwenyezi mungu kwa kufunga Hat Trick ya kwanza kwenye Ligi ya Tanzania.” alisema Mayele.

 

Hadi sasa Mayele ana jumla ya mabao 6 akiwa sambamba na nyota wa klabu ya Simba Moses Phiri pamoja na mshambuliaji wa Namungo FC Reliants Lusajo huku mshambuliaji Sixtus Sabilo akiwa kinara wa mabao hadi sasa akiwa na jumla ya mabao 7.

Leave A Reply