Mayweather awaponda T.I., 50 Cent kwa kuisusia Gucci

 BONDIA Mmarekani, Floyd Mayweather, amewananga wasanii, mastaa, T.I. na 50 Cent, wanaomshambulia kwa kuliunga mkono kampuni la mavazi la Gucci  ambalo linauza vazi maalum linalotumiwa na waigizaji weupe (Wazungu) kuwafanya waonekane wana sura nyeusi.

Katika kuonyesha hawakubaliani na jambo hilo, 50 Cent amechoma moto vitu vyote vya Gucci alivyokuwa navyo, ambapo T.I. na mastaa wengine wameapa kususia bidhaa za kampuni hiyo.

Zaidi ya hapo T.I. ametoa wimbo wa kumzodoa Mayweather ambao ameuita “F##k N##ga.”

Katika kuwashambulia wasanii hao, Mayweather amesema ni wanafiki, watu ambao kazi yao ni kuimba nyimbo zinazosifia madawa ya kulevya, mauaji na ngono, mambo ambayo wanayaeneza katika jamii ya watu weusi huku wakionyesha kwamba wanaipigania na kuijali.

“Mastaa hawa ndiyo baba na waume wakorofi wanaoyatumia majukwaa kupinga bidhaa nzuri lakini wakiwa msitari wa mbele kuharibu jamii kwa nyimbo zao,” aliandika Floyd katika post zake.

Wakati huohuo, bondia huyo ameweka picha yake aliyovaa jaketi la Gucci akiwa katika ndege yake binafsi.

Pia, wakati huohuo,  50 Cent ameendeleza vita yake ya kumpaka matope Floyd akisema akili yake haimtoshi.

Loading...

Toa comment