The House of Favourite Newspapers

MAZIKO YA ERICK KANTONA YAAHIRISHWA

MAZISHI ya mwanamuziki wa Mapacha Music Band inayoongozwa na Jose Mara, Erick Kantona Mugogo wa Mazizini au Msanii wa Bei Kali, aliyefariki usiku wa Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari aliyekuwa azikwe jana,  maziko hayo yameahirishwa.

Mwanamuziki Abdul Misambano akiuliza sababu ya kuahirishwa mazishi hayo.

Mwanamuziki huyo alipatwa na umauti huo alipokuwa akitokea maeneo ya Mbezi jijini Dar alikokuwa akipiga ‘deiwaka’ kwenye baa moja.  Alipokuwa njiani akirudi nyumbani  gari alilopanda liligongana na gari jingine na kumsababishia umauti.

Waombolezaji wakisikiliza kinachoendelea.

Akitoa taarifa za kuahirisha maziko ya msanii huyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (Chamudata) Hassani Msumari,  alisema mpaka kufikia jioni ya saa kumi bado taratibu za Ubalozi wa DR Congo, Polisi na Uhamiaji zilikuwa hazijakamilika na haikuweza kufahamika mara kama zingekamilika muda gani.

 

Hivyo wakaona ni bora waahirishe zoezi hilo na kumzika marehemu huyo kesho jioni kwenye Makaburi ya jijini Dar.

Erick Kantona Mugogo enzi za uhai wake

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL   

Comments are closed.