The House of Favourite Newspapers

Mazoezi ya Yoga ya nchini India kufanyika nchini

0

1.Balozi wa India hapa nchini,Sandeep Arya (katikati) akisoma taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).

Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (katikati) akisoma taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).

2.Balozi Sandeep Arya (wa pilia kushoto) akiwa na  viongozi wengine wa ubalozi huku wakionesha vitabu vyenye michoro ya watu wakifanya mazoezi ya viungo.

Balozi Sandeep Arya (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wengine wa ubalozi huku wakionesha vitabu vyenye michoro ya watu wakifanya mazoezi ya Yoga.

3.Viongozi hao wakionesha baadhi ya fulana zitakazovaliwa siku hiyo ya maadhimisho.

Viongozi hao wakionesha baadhi ya fulana zitakazovaliwa siku hiyo ya maadhimisho ya mchezo wa Yoga.

4.Baadhi ya raia wa nchini India waliopo hapa nchini wakifanya mazoezi kuelekea siku hiyo ya maadhimisho.

Baadhi ya raia wa nchini India waliopo nchini wakifanya mazoezi kuelekea siku hiyo ya maadhimisho.

5.Mazoezi yakiendelea.

Mazoezi ya Yoga yakiendelea katika Ofisi za Utamaduni wa Watu wa India, Masaki jijini Dar.

MAZOEZI ya viungo vya mwili yenye asili ya nchini India (Yoga) yanatarajia kufanyika Juni 19, mwaka huu katika Fukwe za Coco jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya utamaduni wao na kimataifa kwa ujumla.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema kuwa Yogo ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye asili katika falsafa ya Uhindi kwa muda wa miaka mingi.
Sandeep alimnukuu Waziri Mkuu wa India, Shri Narendra wakati akihutubia mkutano wake wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 27, 2014 ambapo alipendekeza  jumuiya ya kimataifa kupitisha siku ya Kimataifa ya Yoga.
Aidha ameeleza kuwa siku ya Yoga siyo tu kufanya mazoezi bali mbinu ya kujitambua na kutambua uhusiano wa mtu na dunia na mazingira yake.
Balozi huyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kufanya mazoezi siku ya Juni 19, mwaka huu kwenye Fukwe za Coco jijini Dar, huku akisisitiza kuwa mazoezi ni uhai wa binadamu hivyo siku hiyo watafundishwa mbinu mbalimbali za kufanya mazoezi ya viungo kutoka kwa wataalam wa nchini India.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply