The House of Favourite Newspapers

Mbao Waja Kuwafurahisha Simba Taifa

Kikosi cha timu ya Mbao FC.

LICHA ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Ruvu Shooting, uongozi wa Mbao ya mkoani Mwanza umeibuka na kusema kuwa wana waheshimu Yanga kama timu kubwa lakini siku ya Jumapili watawasamehe tu kwani watatengeneza matokeo ya kuwafurahisha Simba.

 

Mbao ambao msimu huu wapo vizuri katika ligi kuu kwani katika michezo nane walicheza wameshinda minne na kutoka sare miwili na kufungwa miwili wakiwa na pointi 14 wakishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi alisema ; “Sisi kama Mbao naweza kusema msimu huu tumejipanga haswa kwani ukiangalia msimu uliopita na msimu huu ni tofauti sio kama tumeridhika na pointi hizi hapa tunaendelea kupambana lakini tunajua kuwa ligi msimu huu ni ngumu.”

Comments are closed.