Mbappe Aomba Kuhama PSG

MBAPPESTRAIKA wa Paris St. Germain, Kylian Mbappe inasemekana anataka kuihama timu hiyo. Mbappe mwenye umri wa miaka 20 inaaminika amewasilisha maombi rasmi kwa uongozi wa PSG ya kutaka kuondoka.

Watu wake wa karibu inasemekana ndio wamekuwa wanamshinikiza Mbappe aachane na PSG. Wapambe wake wanaamini kuwa Mbappe anapaswa kuondoka PSG ili aweze kupata changamoto mpya.

 

Mbappe anahesabiwa miongoni mwa wanasoka bora duniani kwa sasa na klabu kadhaa zinataka kumsajili. Mfaransa huyo alidai hivi karibuni kuwa angependa kupata changamoto katika klabu itakayomwamini.

 

Taarifa zinasema kuwa Mbappe alitoa kauli hiyo kuashiria kuwa sasa anataka kupata changamoto mpya kwingineko. Klabu za Real Madrid na Barcelona ndio katika siku za karibuni zimeonyesha nia ya kumnyakua straika huyo


Loading...

Toa comment