The House of Favourite Newspapers

Mbappe wa Serengeti Mambo Safi Denmark

MSHAMBULIAJI tegemeo wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Kelvin Pius John ‘Mbappe’, yupo mbioni kuelekea Denmark kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa ambayo yatachukua takriban wiki tatu.

Kelvin aliibuka kuwa mchezaji bora kwenye mashindano ya kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza Afcon kwa vijana umri chini ya miaka 17 yaliyofanyika hapa nchini, ambapo pia aliibuka kuwa mfungaji bora namba mbili wa mashindano hayo, akitumbukiza wavuni mara saba na kuwa kivutio kikubwa kwa maskauti mbalimbali ambao walianza kumtolea macho kinda huyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, meneja wa mchezaji huyo Mbaki Mutahaba amesema kuwa anashindwa kuweka bayana ni lini ataondoka na timu gani ataenda kujiunga nayo huko Denmark kwa sababu bado wanasubiria majibu ya Visa ambapo kesho Jumanne wanategemea kupata majibu ya ombi lao la Visa na mambo yakiwa sawa, kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo watakuwa na ratiba kamili na kila kitu wataweka wazi.

 

“Jumanne (kesho) tunategemea kupata majibu ya ombi la Visa kwenda Denmark na likipita Kelvin ataondoka Jumatatu ya wiki ijayo kwenda huko kwa wiki kama tatu, tu­nataka kupata uhakika wa Visa kwanza kabla hatujatamka chochote, kwa hiyo naomba uvute subira,” alisema Mutahaba.

Issa Liponda, Dar es Salaam

 

MSIKIE KOCHA WA STARS AKIFUNGUKA HAPA KILICHOTOKEA

Mechi za leo hizi hapa, bashiri na Biko ushinde mkwanja chapchap, bofya hapa ==> BIKO SPORTS

Comments are closed.