Mbaroni Kujiandikisha Zaidi ya Mara Moja

WATU wanne wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kuvuruga uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 baada ya kubainika kujiandikisha katika kituo zaidi ya kimoja.

 

Akizungumza leo Ijumaa Oktoba 11, 2019 mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, amesema watuhumiwa hao walikamatwa jana Alhamisi katika vituo vya kata ya Ngamiani Kusini na Ngamiani Kati na kwa sasa wanahojiwa na polisi.

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi Wilaya ya Tanga, Ramadhani Posi, amesema leo saa sita  mchana wakazi 44,615 wamejitokeza katika vituo 498 sawa na asilimia 34 ya wakazi 135,892 wanaotarajiwa kujiandikisha.


Loading...

Toa comment