The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mbaroni kwa Kuuza Mtoto kwa Sh. 3,000

0

 

MSICHANA wa miaka 17, mama yake na mwanamke mwingine wamekamatwa na polisi kwa kumuuza mtoto mchanga kwa  Sh3,000.

 

Hilo limetokea huko Butere, ambako msichana huyo aliyekuwa anasoma shule alifukuzwa na baba yake baada ya kupata mimba na hivyo kwenda kuishi kwa mama yake.

 

Baba yake alimfukuza akidai kwamba kwa vile aliupata ujauzito huo kutoka kwa mpwa wake na kwamba watoto wanaozaliwa katika njia hiyo ni haramu kwa jamii yao.

 

Hata hivyo, wazee walisema suluhu ya watoto watokanao na mimba hizo ni kufanyiwa taratibu za kisheria za “kuwasafisha” na si kuwaua au kuwafukuza.

 

Mama wa msichana huyo alidai kwamba mumewe waliyetalikiana naye alitaka mtoto huyo auawe lakini yeye aliamua kumuuza kwa vile hakuwa na hela ya kumlea mjukuu wake huyo.

Leave A Reply