The House of Favourite Newspapers

MBASHA AMFUNGUKIA WEMA SEPETU

Image result for Emmanuel Mbasha
Emmanuel Mbasha

MSANII wa Muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu ishu inayoendelea sasa hivi mitandoni kuwa nani ni Tanzania Sweetheart (Kipenzi cha Watanzania) kati ya mrembo Wema Sepetu na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Akizungumza na Ijumaa, Mbasha alisema kuwa kwa upande wake, Tanzania Sweetheart kati ya warembo hao wawili, ni Wema kwani ndiye anayestahili.“Hilo jina linamfaa aliyekuwa nalo tangu zamani (Wema), kwani ndiye aliyepewa hilo jina, kwa hivyo acha tu aendelee nalo kwa sababu ndio linampendezea,” alisema Mbasha.

Stori: Memorise Richard

Comments are closed.