MBASHA AMTUPIA ‘DONGO’ MC PILIPILI
BAADA ya mshereheshaji Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ kujitamba mtandaoni kwa kuweka picha zake akiwa na mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Qute Mena, msanii wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha, ‘Mbasha’ amemtupia dongo MC huyo kwa kumwambia kuwa amekiuka taratibu za dini. Akizungumza na Ijumaa, Mbasha alisema lengo la kumuandikia ujumbe mrefu MC Pilipili kwenye ukurasa wake wa Instagram, lilikuwa ni kumjenga pamoja na kumuelimisha kwamba kitendo anachokifanya sio sahihi.
“Unajua sio vizuri kumuanika wazi wazi mchumba wala kuwa naye karibu kiasi ambacho hata watu wakiwaona watashangaa, kwa sababu tunafundishwa kwamba, ukishamchumbia mtoto wa kike hutakiwi kufanya naye kitu chochote mpaka pale utakapo muoa na kumfanya mke wako.
“Sasa Napata wasiwasi kwa huyu ndugu yangu MC Pilipili na huyo mchumba wake, nimepata taarifa kwamba wapo Zanzibar sasa sijajua kama wamechukua vyumba tofauti au wanaishi kwenye chumba kimoja, kitendo ambacho si kizuri, ila lengo la kumuandikia ule ujumbe kwenye akaunti yangu ni kumuelisha kwa sababu yeye ni kioo cha jamii na watu wanahitaji kujifunza kutoka kwake,” alirusha dongo Mbasha.
Ijumaa lilimtafuta MC Pilipili kuzungumzia upande wake ambapo simu yake iliita kwa muda bila kupokelewa na baada ya kutumiwa ujumbe mfupi alijibu kuwa atapiga baadaye jambo ambalo hakulitekeleza.
Stori: Memorise Richard
Comments are closed.