Mbasha apotezea talaka kisa Magufuli

ema-mbasha
Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara maarufu Bongo, Emmanuel Mbasha

Gladness Mallya

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara maarufu Bongo, Emmanuel Mbasha amepotezea kuzungumzia suala la kumpa talaka mkewe kwa madai kwamba yupo bize na suala la sherehe za ushindi wa rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli.

mbasha2Aliyekuwa mke wa Emmanuel Mbasha, Flora Mbasha

Mbasha aliitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati mwanahabari wetu alipomuuliza mwimbaji huyo kuhusu hatma ya kutoa talaka ambayo aliyekuwa mkewe, mwimbaji Flora Mbasha amekuwa akiidai hadi kumfikisha mahakamani.

mbashaEmmanuel Mbasha na mkewe

“Sikia bwana, mimi kwa sasa nipo bize na sherehe za ushindi wa Magufuli siwezi kupoteza muda wangu kuzungumzia vitu vidogovidogo kama hivyo, kwangu mimi rais wa nchi ni muhimu kuliko hayo mambo ya Flora unayoniulizia,” alisema Mbasha.

Emmanuel na Flora walikuwa wanandoa na kubarikiwa kupata mtoto mmoja kisha kugombana na kufikia hatua ya kuachana na sasa kila mmoja anaishi kivyake.


Loading...

Toa comment