The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Akabidhi Faili La Usajili

0

WAKATI ligi ikiwa imesimama kutokana na Virusi vya Corona, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amekabidhi faili la usajili wa msimu ujao kwa mabosi wake huku jina la kiungo wa Yanga, Mkongomani Papy Tshishimbi likiwa si miongoni.

 

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa raia wa Afrika Kusini, amesema kuwa kwenye kipindi hiki tayari kocha huyo ameshawapa majina ya wachezaji ambao anawataka katika kikosi hicho kwa msimu ujao huku pia akiainisha kina nani waachwe huku wakiweka bayana kwamba hawatamkosa mchezaji yeyote katika orodha hiyo.

Senzo ameongeza kuwa katika orodha ya majina ambayo wachezaji wametakiwa kwa ajili ya msimu ujao jina la Tshishimbi halimo na wala hawakuwa wanamhitaji tofauti na ilivyokuwa inatajwa.

 

Msauz huyo amesema kwamba tayari wanayo majina ya wachezaji ambao watakuwepo kwenye kikosi hicho kwa msimu ujao baada ya kocha huyo kuwapa faili zima la nani anamhitaji kwenye kikosi chake na nani hamtaki.

 

“Kocha ametupa majina yake juu ya nafasi gani ambazo anaona zisajiliwe kwa msimu ujao, pia nani atamaliza ligi na kina nani tuachane nao. Pia kuna wale ambao anataka kuwa nao kwenye pre-season ya msimu ujao.

 

“Tunaamini juu ya wachezaji wote ambao wanatakiwa basi tutakuwa na uhakika mkubwa wa kuwapata, hakuna ambaye atakuwepo na tukashindwa kumpata. “Juu ya Tshishimbi hatukuwa tunamhitaji, hatukusema tunamhitaji yeye, ana timu anayoichezea na tunaliheshimu hilo,” alisema Senzo.

SPOTI HAUSI: SAKATA la LIGI KUFUTWA / MAKAMBO Kurudi YANGA / GSM KUJIONDOA…

Leave A Reply