The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Autambulisha Mfumo Wa TP Mazembe Yanga Sc

0

UNAKIKUMBUKA kikosi cha Yanga kilichoiua Simba bao 1-0 pale Uwanja wa Taifa Jumapili iliyopita, Kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael amesema mfumo alioutumia ndio chanzo cha mafanikio yao kwa sasa.

 

Katika mchezo huo, Yanga ilitumia mfumo wa viungo watano na mshambuliaji mmoja, huku kocha huyo akisema mfumo huo ndiyo uliwapa matokeo chanya TP Mazembe ya DR Congo mwaka 2010.

 

Yanga katika michezo ya hivi karibuni kwenye Ligi Kuu Bara ukiwemo dhidi ya Simba, ilitumia mfumo huo kwa kuwaanzisha Papy Tshishimbi, Feisal Salum, Haruna Niyonzima, Balama Mapinduzi na Bernard Morrison, huku mbele akisimama Ditram Nchimbi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Eymael alisema kuwa, kutumia kwake viungo wengi ni kutokana na hazina ya ubora wa viungo wanaopatikana katika kikosi chake.

Kocha huyo alisema mfumo huo ndiyo ule uliokuwa ukitumiwa zaidi na TP Mazembe mwaka 2010 na kufanikiwa kutesa Afrika ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akitangaza kuendelea kuutumia katika michezo ijayo.

 

“Kikosi changu kina viungo wengi wazuri, ninafurahia uwepo wao, nikiwaangalia naikumbuka TP Mazembe ya mwaka 2010 wakati ninafundisha AS Vita ya DR Congo. Walikuwa wakiutumia mfumo huo katika baadhi ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na walifanikiwa haswa.

“Kikubwa timu ya ushindi huwa haibadilishwi sana, hivyo naweza nikaendelea kuutumia mfumo huu kutokana na aina ya wapinzani ambao tutakuwa tunakutana nao.

 

“Lakini katika mfumo huu unatakiwa uwe na mshambuliaji ambaye yupo fiti sana kwa ajili ya kupambana kisawasawa,” alisema kocha huyo.

STORI NA MARCO MZUMBE

MASHABIKI WA SIMBA Waivaa YANGA Baada ya Kuipiga SINGIDA 8 ,Waitaka FA SIMBA VS YANGA

Leave A Reply