The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji awashtukia Vita

 

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ametamka kwamba anaelewa mechi yao na AS Vita itakuwa ngumu kutokana na wenzao kufungwa mechi yao ya kwanza, hivyo hataenda kizembe badala yake watajiandaa kikwelikweli.

 

Mbelgiji huyo wikiendi hii ataiongoza Simba kwenye mechi ya pili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya AS Vita ya DR Congo.

Ikumbukwe kwamba Simba hii ni mechi yao ya pili ya hatua hiyo baada ya ile ya kwanza waliyocheza na JS Saoura na kushinda mabao 3-0.

 

Kocha huyo ameliambia Championi Jumatano, kuwa anajua mechi hiyo itakuwa ngumu kwao kutokana na wenzao kuwa nyumbani lakini pia watataka kupata pointi tatu baada ya kupoteza mechi yao ya kwanza jambo ambalo linawafanya wao wajipange kikamilifu.

 

“Najua mechi hii itakuwa ngumu kwetu kwa sababu kwanza tunaenda ugenini lakini pia Vita wenyewe walifungwa mechi ya awali hivyo watataka kufanya vizuri wakiwa kwao.

 

“Kwa maana hiyo tumeweka mikakati ya kujiandaa kikamilifu kupambana nao na tumejiandaa vyema tu kuhakikisha kwamba hatupotezi pointi kirahisi, tunataka kushinda kama ikishindikana basi iwe sare na siyo kufungwa,” alisema Mbelgiji.

 

Comments are closed.