The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Awaweka Viporo Ajibu, Kichuya Simba

0

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji, ameweka wazi kuwa, kutokana na upana wa kikosi alichonacho kwa sasa ndani ya timu, itawalazimu baadhi ya nyota kama Ibrahim Ajibu na Shiza Kichuya kuhakikisha wanapambana ili wapate nafasi kwenye kikosi chake.

 

Kocha huyo tangu atue kikosini hapo, amekuwa akiwatumia nyota tofautitofauti kulingana na aina ya wapinzani ambao atakutana nao katika mashindano mbalimbali. Akizungumza na Championi Jumamosi, Sven alisema amechoshwa kusikia baadhi ya watu wakilalamika kitendo cha yeye kutowatumia nyota kama Ajibu na Kichuya katika kikosi chake kwani yeye anajua nini anachokifanya.

“Simba ina wachezaji wengi wazuri katika kila idara, hivyo ili mchezaji upate nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza, lazima unishawishi kwanza mimi mwalimu, hivyo kama kuna wachezaji

hawaanzi kila mara kwenye kikosi changu, wanatakiwa wapambane kuhakikisha wanapata nafasi. “Mimi sipangi timu kwa mazoea, huwa namfuatilia mchezaji kuanzia mazoezini hadi uwezo aliouonyesha katika mchezo uliopita, hivyo kama atafanya vyema sehemu zote hizo lazima nimtumie katika kikosi changu,” alisema kocha huyo

Leave A Reply