Mbelgiji Simba Aichimba Mkwara Namungo

WAKATI zikiwa zimebaki saa chache kabla ya fainali ya Kombe la Shirikisho, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amefunguka licha ya maandalizi waliyokuwa nayo kwa siku kadhaa lakini anaona Uwanja wa Nelson Mandela unaweza kumuharibia.

 

Kocha huyo ameongeza kuwa, licha ya yote hayo lakini bado hesabu zake zote ni kuhakikisha kwamba ubingwa wa kombe hilo anautia mkononi.

 

Sven ataiongoza Simba, kesho Jumapili kupambana na Namungo FC kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo itapigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji ameliambia Championi Jumamosi kuwa, uwanja huo unaweza kuwa kikwazo kwao kutokana na kutokuwa sawa kwa asilimia 100 lakini hawana namna zaidi ya kupambana na wapinzani wao.

 

“Hii ni mechi muhimu kwetu na tumekuwa na maandalizi nayo kwa kipindi kirefu, tukianzia na zile mechi mbili za mwisho za ligi kabla ya kwenda Mbeya “Itakuwa ngumu na tunatakiwa kujiweka sawa zaidi kuliko wapinzani kwa sababu ya wapinzani wetu walivyo lakini pia aina ya uwanja ambao tutauchezea.

 

“Uwanja siyo mzuri sana lakini hakuna namna zaidi ya kupambana kwa sababu lengo letu tunalolitaka ni kuona tunashinda ubingwa huu kama ambavyo tumekuwa tukitamani kuona tunafanikisha hilo,” alimaliza Sven.

STORI: Said Ally Dar es Salaam

Toa comment