The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Simba Aja na Mikakati ya Ubingwa

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, baada ya kucheza mechi mbili za kirafiki, amefunguka kuwa anataka kuona wachezaji wanakuwa imara kwa kumudu kucheza nafasi zaidi ya moja kutokana na aina ya mifumo ambayo amepanga kutumia itakuwa miwili au mitatu.

Aussems amesema anatarajia kuwa na mifumo miwili au mitatu mipya ambayo ataitumia msimu ujao.

 

Kocha huyo kwa sasa yupo bize kukinoa kikosi chake hicho kipya, kwa ajili ya msimu mpya ambacho kimesheheni nyota 11 wapya wa ndani na wa nje.

Patrick Aussems

Msimu uliopita, Aussems alitumia mifumo miwili zaidi, ule wa 3-5-2 hasa kipindi Shomari Kapombe akiwa fiti lakini baadaye alitumia zaidi ule mfumo wa 4-4-2.

 

Aussems amesema anahitaji kuona wachezaji wake wanakuwa bora uwanjani na kumudu kucheza nafasi zaidi ya moja ili kuweza kuendana na mifumo ambayo amepanga kutumia, miwili au mitatu.

 

Kocha huyo kwa sasa anaandaa kikosi chake kwa ajili ya mechi ile ya kwanza ya kimataifa ambayo itachezwa kati ya Agosti 9-11, mwaka huu kabla ya ligi kuanza dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, ikianzia ugenini.

Aussems alisema: “Nataka kuona wachezaji wangu wakicheza nafasi zaidi ya moja, sababu msimu ujao nataka kuwa na mifumo miwili au mitatu.”

 

Hata hivyo, Aussems hakufafanua zaidi kuhusu mifumo hiyo. Simba katika maandalizi yake hayo imefanikiwa kucheza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Platinums Stars (ilishinda mabao 4-1) huku ikicheza na Orbret TVET na kushinda 4-0.

 

Kesho Jumamosi, Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Township Rollers ya Botswana ambayo itavaana na Yanga katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi ujao.

Comments are closed.