The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Simba Awaota Wakongo wa Zahera

Mbelgiji, Patrick Aussems.

KOCHA mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa hawazi kupata ushindi katika mechi yake na JS Saoura bali anaumiza kichwa jinsi ya kuifunga AS Vita inayonolewa na Florent Ibenge ambaye ni swahiba mkubwa wa Mwinyi Zahera wa Yanga.

 

Simba ambayo iko nafasi ya pili katika kundi D, ikiwa na pointi sita, nyuma ya vinara wa kundi hilo, Al Ahly ya Misri wenye pointi saba wakat JS Saoura kutoka Algeria ikiwa na pointi tano huku As Vita ya DR Congo ikiwa na pointi nne.

 

Simba inaondoka Dar es Salaam Jumanne ambapo Jumamosi itacheza na JS Saoura ugeninikabla ya kuvaa na AS Vita Machi 16.

Akizungumza na Spoti Xtra, Aussems alisema; “Nilisema mapema hili kundi lipo wazi sasa na kila mmoja anaona hali halisi sasa tupo wapi na tunayo nafasi kubwa ya kwenda robo fainali kama tutafanikiwa kuifunga AS Vita hapa kwetu.”

 

“Na ndiyo jambo kubwa ninalolipa nafasi kubwa kwenye akili yangu kuelekea kwenye mchezo huo. “Matumaini yangu yapo kwenye mechi na As Vita siyo wale JS Saura labda pengine itokee sare lakini sioni dalili za kuweza kufanya hivyo kwa sababu soka la Afrika limekuwa na mambo mengi hasa kwa upande wa timu mwenyeji ndiyo maana najipanga na As Vita kufanya kile ambacho tuliweza kufanya kwa Nkana,” alisema Aussems.

Comments are closed.