visa

Mbelgiji Simba: Hakuna Shoo Simba, Nataka mabao

Patrick Aussems amewapiga biti wachezaji wa kikosi hicho kwa kuwaambia hataki kuona wakicheza mpira wa shoo badala yake anataka kuwaona wanafunga mabao ya kumwaga. Simba wiki iliyopita ilianza Ligi kwa kuwapiga JKT Tanzania mabao 3-1 Jijini Dar es Salaam.

 

Mbelgiji huyo ameliambia Spoti Xtra, kuwa aliona jambo hilo katika mchezo huo ambao walistahili kushinda mabao mengi lakini kutokana na uchezaji wa shoo na utoto ndani wakashindwa.

 

“Tulikuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda mabao matano kwenye mechi yetu na JKT Lakini tulishindwa kwa sababu wachezaji walicheza kitoto.

 

“Walikosa nafasi ya kufunga mabao hayo ya wazi, kwangu mimi sikubaliani na hali hiyo na tunatakiwa kubadilika na kuhakikisha kwamba tunafunga mabao mengi katika kila nafasi ambayo tunaitengeneza katika mechi zetu,” alisema Aussems amefeli mtihani wa kwanza kimataifa.

SAID ALLY, DAR
Toa comment