The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Yanga Aahidi Mabao Kila Mechi

0
Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Ubelgiji, Luc Eymael.

KOCHA Mkuu wa Yanga raia wa Ubelgiji, Luc Eymael, amesema kuwa kutokana na jinsi kikosi hicho kinavyofanikiwa kupata nafasi nyingi za kufunga mabao, ana uhakika baada ya mechi tano zijazo kitakuwa kikifunga mabao mengi zaidi.

 

Eymael amejiunga na Yanga hivi karibuni baada ya timu hiyo kuachana na Mwinyi Zahera aliyefungashiwa virago Novemba, mwaka jana.

Juzi Jumatano, kocha huyo ilikuwa ni mechi yake ya tatu tangu ajiunge na Yanga wakati walipocheza dhidi ya Singida United na kushinda 3-1 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.

 

Kabla ya hapo, alipoteza mechi mbili kwa Kagera Sugar, Yanga ilifungwa mabao 3-0 kisha ikachapwa tena na Azam FC bao 1-0.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Eymael alisema kuwa, kwa namna anavyokiona kikosi hicho, ana uhakika baada ya mechi tano zijazo atakuwa akipata mabao mengi zaidi kwani kwa sasa bado anaendelea kutafuta muunganiko mzuri wa timu ambayo pia inampa matumaini kutokana na kutengeneza nafasi nyingi.

 

“Timu yangu iko safi na kwamba ninajua tumetoka kupoteza mechi mbili zilizopita ila namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata ushindi wa kwanza kwa idadi hii ya mabao huku wachezaji wangu wakikosa nafasi nyingi za mabao, jambo ambalo naamini siku zijazo nitakuwa nimelimaliza,” alisema Eymael.

Leave A Reply