The House of Favourite Newspapers

MBEYA: Askari 2 Wafariki kwa Ajari, 9 Wajeruhiwa

IYUNGA, MBEYA: Askari wawili wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutiliza Gjasi (FFU) wamefariki na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari aina ya Defender kupata ajali wakati wakielekea lindoni.

Ajali hiyo imetokea leo Januari 18, 2018 majira ya saa 10:45 jioni maeneo ya Iwambi barabara ya Mbeya Tunduma, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Mkoani wa Mbeya.

Imeelezwa gari hilo lenye namba za usajili PT.2079 Landrover, mali ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia  Mkoa wa Mbeya likiendeshwa na askari namba G.3452 PC Adam miaka 30, wakati likiwa linapeleka askari kazini iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya askari wawili huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni mwendokasi.

Askari waliopoteza maisha ni;

  1. H.1215PC Prosper s/o Jordan Chalamila miaka 29, wa FFU Mbeya na
  2. H.4335 PC Mathew s/o Jailos Mpogole miaka 26, wa FFU Mbeya

Askari wengine 9 wamejeruhiwa ambapo kati yao watatu wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya;

  1. G.3452 PC Adam miaka 30, ambaye ameumia maeneo ya kifua
  2. G.6849 PC Khamis Ally miaka 32, ambaye ameumia maeneo ya kichwani.
  3. H. 6952 PC Kelvin s/o Martini miaka 28, ambaye ameumia maeneo ya kichwani/ usoni

Askari wengine 06, wametibiwa na kuruhusiwa ambao ni;

  1. H.3929 PC Leonard Michael miaka 26, Alipata jeraha mkono wa kushoto.
  2. H.469 PC Fredy Mbande miaka 28, alipata jeraha mgongoni.
  3. H.948 PC David Ibrahim miaka 27, alipata maumivu ya mwili.
  4. G.9588 PC Marwa Itembe miaka 29, Alipata maumivu ya mwili.
  5. H.1325 PC Christopher Daniel Msangi miaka 26, alipata maumivu ya mbavu.
  6. H.6789 PC Lucas Andrea Mashala miaka 24, ambaye alipata jeraha kichwani kulia na maumivu ya mbavu kulia.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Comments are closed.