Mbeya City Kamili Kuwakabili Simba
BAADA ya Bodi ya Ligi kutangaza mabadiliko ya ratiba kwa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Bara, Wagonga Nyundo wa Jiji la Mbeya, Mbeya City wamesema wapo kamili kuwakabili Simba.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Januari 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa
ambapo awali ulikuwa haukupangiwa tarehe.
Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha wa Mbeya City, Mathias Lule, amesema wamejiandaa vema
kuhakikisha wanafanya vizuri.
“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, tumejiandaa vizuri kuwakabili Simba na tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kutupa sapoti,” alisema.
STORI: DERICK LWASYE, MBEYA