Mbeya City yajitosa kwa Atupele, Seseme
Hans Mloli, Dar es Salaam
VUGUVUGU la usajili na kuimarisha vikosi kwa ajili ya msimu ujao tayari limeanza ambapo mapema Mbeya City imeanza kwa kufukuzia saini za mshambuliaji wa Ndanda FC, Atupele Green na kiungo wa Toto Africans, Abdallah Seseme.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa, Mbeya City sasa inahitaji zaidi kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo kwa ajili ya kuja kusaidiana na Kenny Ally, hivyo mtu sahihi akaonekana ni Seseme aliyewahi kuitumikia Simba SC kabla ya kutimkia Toto mwanzoni mwa msimu huu.
Mtu wa ndani kutoka Mbeya City amelieleza Championi Jumatano kuwa, ujio wa Atupele aliyefunga mabao 10 mpaka sasa umechagizwa kwa kukosekana straika mwenye njaa ya kufunga kikosini hapo kama ilivyokuwa mwanzo kwa Mwegane Yeya.
“Ukiachana usajili wa Wamalawi, kuna Seseme naye anahitajika kwa ajili ya kuja kuimarisha kiungo lakini pia Atupele kazi yake inaonekana, atakuja kuongeza mashambulizi maana kwa msimu huu tulikuwa na tatizo hilo,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe kuzungumzia suala hilo, alisema: “Bado hatujaanza usajili kwa sasa, nafikiri baada ya mechi yetu ya mwisho ya ligi ndiyo tunaweza kuanza kuongelea masuala hayo tukishapata ripoti ya mwalimu.”
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz