The House of Favourite Newspapers

Mbeya Kwanza Wakubali Kuwapa Yanga Straika

0

WAKATI kukiwepo na tetesi za Yanga kumuhitaji straika Chrispin Ngushi, mabosi wa straika huyo Mbeya Kwanza wameibuka na kubainisha kuwa wapo tayari kumuachia nyota huyo kutua Jangwani.


Ngushi amekuwa na msimu
mzuri hadi sasa akiwa na Mbeya Kwanza ambapo ameweka kambani mabao matatu na asisti moja.


Akizungumza na
Championi Jumamosi, Mwenyekiti wa Mbeya Kwanza, Mohammed Mashango alisema kuwa endapo Yanga watakuwa tayari kwa ajili ya mazungumzo basi wao kama timu watamuachia mchezaji huyo.


“Hadi sasa bado hatujapata
ofa yoyote kutoka kwa Yanga lakini tumekua tukisikia kuwa wanamuhitaji lakini bado hawajafika kwetu kama wakija tukafanya mazungumzo na tukafikia makubaliano mazuri basi kila kitu kitakuwa wazi.


“Sisi kama timu tupo tayari
kumuachia Chrispin kwenda Yanga kwani lengo letu ni kuona vijana wetu wanakuza vipaji, kwa hiyo hatutakuwa na pingamizi kwenye jambo hilo,” alisema Mashango.

HAWA ABOUBAKHARI, Dar es Salaam

Leave A Reply