Mbezi High School Waipokea kwa Shangwe Jipange na Pepa

Wanafunzi wa Mbezi High School wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Jipange na Pepa.

Project ya Jipange na Pepa, inazidi kupasua anga ambapo leo, Jumatano, Februari 12, 2020, imefanyika katika Shule ya Sekondari ya Mbezi Beach High School na kutambulishwa kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo, waliyoipokea kwa shangwe.

Mratibu wa Jipange na Pepa, Aziz Hashim akizungumza na wanafunzi.

 

“Tumefurahi sana kugundua kwamba kumbe kwenye magazeti ya Global Publishers kuna mitihani kwa ajili yetu. Napenda sana Mathematics na nimefurahi kukuta mitihani na majibu yake kwenye Gazeti la Risasi,” alisema mmoja kati ya wanafunzi waliozungumza na mwandishi wetu.

Hashim akifafanua jambo mbele ya wanafunzi. Kulia kwake ni Elvan Stambuli, Mhariri Mwandamizi wa Global Publishers na Anthony Adam, Afisa Masoko GPL.

 

“Tunawashukuru sana Global Publishers kwa kuja na project hii, hakika itawasaidia sana wanafunzi kuzoea mitihani na hivyo kuwa na uwezo wa kufanya vizuri kwenye mitihani ya taifa,” alisema George William, mmoja kati ya walimu wa shule hiyo.

 

Akizungumza na mamia ya wanafunzi waliofurika kwenye Ukumbi wa Kiramuu uliopo shuleni hapo, mratibu wa Jipange na Pepa, Aziz Hashim amesema mitihani iliyotungwa na walimu wazoefu kwa kufuata mfumo wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), huchapishwa katika magazeti ya Global Publishers kwa lengo la kuwajengea wanafunzi uwezo.

 

 

“Mitihani ya masomo ya Biology, History, Kiswahili, English, Mathematics, Civics, Chemistry, Physics na Geography huwachapishwa kwenye magazeti ya Uwazi, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Ijumaa huku majibu ya kila mtihani yakitolewa kwenye toleo linalofuatia la gazeti husika.

 

Mmoja kati ya wanafunzi wa Mbezi High School akijibu swali la papo kwa hapo.

 

“Kwa kila wiki, mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kujipima kwa kufanya mtihani karibu kila siku na kumfanya azoee mitihani na kuondokana na hofu inayosababisha wengi wapanic wakiwa kwenye vyumba vya mitihani.

Hashim akimuongoza mwanafunzi kujibu maswali ya papo kwa hapo.

“Mitihani hii pia itamfanya mwanafunzi aelewe jinsi maswali yanavyoulizwa katika kila somo na kuongeza uelewa wake kitaaluma,” alisema Hashim.

Baadhi ya wanafunzi wakijibu maswali ya Somo la Mathematics kutoka kwenye Gazeti la Risasi Mchanganyiko.

 

Mbali na kutambulishwa project hiyo, wanafunzi waliojibu maswali ya papo kwa hapo yaliyoulizwa, pia walijinyakulia zawadi za papo kwa hapo ikiwemo madaftari na vifaa vingine vya kusomea na kuwafanya wafurahi sana.

 

 

“Tunaomba muwe mnakuja mara kwa mara, nimefurahi sana kupewa zawadi ya madaftari, rula na peni kwa kujibu maswali ya papo kwa hapo,” alisema mwanafunzi mwingine aliyekuwa miongoni mwa washindi.

 

Ni wakati wa zawadi! Mwanafunzi aliyejibu vizuri maswali ya papo kwa hapo akikabidhiwa zawadi na Elvan Stambuli, Mhariri Mwandamizi Global Publishers.

Stambuli akikabidhi zawadi

Zawadi zinaendelea kutolewa

Afisa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam akikabidhi zawadi.

Wanafunzi wakigombea zawadi ndogondogo.

Mmoja kati ya wanafunzi akizungumza na Global TV Online kuhusu namna alivyoipokea Jipange na Pepa.

 


Loading...

Toa comment