The House of Favourite Newspapers

MBINU ZA KUKABILIANA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME-2

WIKI iliyopita tulianza kuangalia tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume ambalo linatajwa kushamiri kwa wanaume wengi. 

 

Kwa mujibu wa mwanafalsafa maarufu wa karne zilizopita, Shake Spear, katika suala la mapenzi, pombe huamsha hisia na hamasa za kushiriki tendo, lakini huondoa uwezo wa kulitenda tendo hilo (alcohol provokes desire but takes away the performance).

 

Kwa kawaida pombe husababisha kusinyaa kwa mfumo wa mishipa ya fahamu (alcohol is a nervous system depressant) na kusababisha kuondoa msisimko wa kimapenzi hata kama una hamu ya kutosha. Pombe, ili kuleta athari mwilini haihitaji unywe kiwango kikubwa, hata glasi mbili tu, zinaweza kuharibu mfumo wa fahamu na ini.

Athari za ini kutokana na pombe huwa haitokei moja kwa moja, huanza taratibu na kusababisha vichocheo au homoni za kike mwilini mwa mwanaume kuwa juu na kushusha homoni za kiume (testosterone) hivyo kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kupunguza hisia za kufanya tendo la ndoa na hata ulevi ukikuzidi huweza kukubadilisha hisia zako na kujikuta unatamani kuingiliwa kimwili.

 

Pombe pia huathiri mishipa ya fahamu. Ili uume uweze kusimama inatakiwa kuwepo na msukumo mkubwa wa damu katika uume. Uume ni kiungo chenye mishipa mingi ya damu (penis is a vascular organ). Endapo sehemu za mishipa hii itaziba, basi uume hauwezi kusimama.

 

Tatizo la kusinyaa kwa mishipa ya damu ya uume hutokea zaidi kwa wanaume wenye umri wa chini ya miaka 40. Ni vizuri kuangalia vyakula unavyokula, vinywaji na hali ya maisha kwa jumla ili kuepuka kuwa na kiwango kikubwa cha cholesterol au lehemu kwenye damu kwani huchangia kuziba au kusinyaa kwa mishipa ya damu hasa ya uume na kuishiwa nguvu za kiume.

 

Pamoja na uvutaji wa sigara kuathiri moyo, tafiti zinaonesha kwamba, nicotine iliyopo kwenye tumbaku husababisha mishipa ya damu kusinyaa, athari za tumbaku kuathiri na kuondoa msisimko kwa hiyo utajikuta una hamu, lakini nguvu hakuna au uume unasimama kidogo halafu unalala.

Uzito mkubwa au unene uliopitiliza husababisha kupunguza uwezo wa kushiriki tendo la ndoa hasa kama uzito wako umeongezeka kwa zaidi ya asilimia ishirini ya uzito wako wa kila siku. Unashauriwa kupunguza uzito kwa kufanya mazoezi na kudhibiti ulaji uzito unaomudu utakupa hali ya kujiamini. Ili kuweza kuwa na ubora katika tendo hili na kuepuka upungufu, inashauriwa kushiriki tendo hili mara kwa mara.

 

Kwa mwanaume mwenye umri wa miaka 55 hadi 75 inashauriwa ashiriki tendo la ndoa siyo chini ya mara mbili kwa wiki kuliko kutoshiriki kabisa au kwenda chini ya hapo. Tafiti zinaonesha kwamba, mwanaume wa umri huu mkubwa akiwa anashiriki tendo la ndoa mara mbili au zaidi kwa wiki huwa vizuri zaidi kuliko yule ambaye hashirki kabisa. Kushiriki huku ni kwa kutotumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.

 

Kupumzika (relaxation), inashauri upate muda mzuri wa kupumzisha akili na mwili. Jitahidi angalau kwa siku upate saa sita za kupumzika na ikibidi kwa wiki upate hata siku moja nzima na angalau basi kwa mwaka mwezi mmoja. Mapumziko hayo yataboresha akili na mwili na nguvu zako kubaki kama kijana. Akili hupumzishwa kwa kulala na kupata burudani siyo kulewa.

 

Inashauriwa pia kushiriki mazoezi ya viungo na furaha kwa jumla, pamoja na mazoezi ya kuboresha mwili, lakini pia husaidia kupunguza maumivu ya mwili kutokana na kuuwezesha ubongo kutoa kemikali iitwayo (endorphins) inayosambaa katika mfumo wa mishipa ya fahamu na kutuliza maumivu kisha kuondoa msongo wa mawazo. Kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara au mara nyingi husaidia sana kuboresha nguvu za kiume na kupunguza maumivu ya mwili na msongo wa mawazo. Mwanaume ambaye hashiriki mara kwa mara hupata tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume.

USHAURI

Endapo una tatizo kama hili, basi unashauriwa uwaone madaktari bingwa wa matatizo ya afya ya uzazi kwa uchunguzi wa kina na matibabu. Usitumie dawa za kuongeza nguvu bila ushauri wa daktari.

Comments are closed.