The House of Favourite Newspapers

Mbinu Za Kumfurahisha Mpenzi Wako Muwapo Faragha

TENDO la ndoa (kwa wa­nandoa) si tu linatumika kuboresha uhusiano kati ya mume na mke bali pia ni dawa inay­oweza kuutibu mwili, akili na hisia. Hata hivyo, lazima liwe ni tendo lililokamilika, kwa maana lazima mwanaume na mwa­namke wote walifu­rahie na kuridhika.

 

Tendo hili lisipofanyi­ka kwa ukamilifu wake, hubadilika na kuwa kero kubwa na janga kwa wanandoa. Kama ambavyo nimekuwa ni­kieleza mara kwa mara, sidhani kama yupo mtu ambaye hataki kumfu­rahisha mwenzi wake wawapo faragha.

 

Tatizo ni kwamba wen­gi hawana maarifa ya nini cha kufanya awapo faragha na mwenzi wake, na matokeo yake wamekuwa wakijiendea wana­vyoweza, kama kutembea kwenye giza totoro usiku wa manane.

 

Hakuna mahali ambapo unaweza kufundishwa namna ya kumfurahi­sha mumeo au mkeo, angalau ki­dogo wazee wetu enzi zao walikuwa wanapelekwa jandoni na unyagoni, siku hizi unakuja kujifunzia ndani ya ndoa, yaani kama ni mechi ya mpira wa miguu basi unajifunzia kutuliza mpira na kupiga danadana uwanja­ni wakati wa mechi ambayo ni lazima ushinde.

 

M f a n o mwepesi am­bao huwa nap­enda kuutumia ni kwamba kila mtu anaweza kuwa anata­mani kupiga gi­taa na kuzalisha muziki mzuri, la­kini hebu jiulize, kama hujawahi kujifunza kupiga gitaa na ukaelewa, ukipewa gitaa sasa hivi unaweza kupiga na kutoa muziki mzu­ri? Jibu ni HAPANA.

 

Mapenzi ni sanaa, lazi­ma ukubali kujifunza na kuyatafuta maarifa ma­hali popote yalipo ili uwe bora, huyo uliyenaye unaweza kuwa unafanya kila kitu kwa ajili yake, unajitahidi kumuonye­sha upendo wa hali ya juu lakini kama hujui nini cha ku­fanya muwapo faragha ili afu­rahi, ni sawa na kazi bure. Ni kwa msingi huo ndiyo maana nikaamua tujadiliane mada hii kama inavyojieleza hapo juu.

 

MAANDALIZI YA KIHISIA

Jambo la kwanza ambalo una­takiwa kulifahamu, ni kwamba ili mume au mke afurahie tendo muwapo faragha, lazima awe ametulia kihisia. Haiwezekani mmetoka kukwazana kuhusu jambo fulani, hamjapata suluhu na kila mmoja ana hasira halafu ndiyo mnaingia uwanjani, hamu­wezi kufurahia tendo kwa mtindo huo na hii inawahusu wote.

 

Maandalizi mazuri ya tendo yanaanzia katika maelewano, mpokee vizuri kwa maneno yaliyojaa bashasha, kwa sauti ya upole, mbembeleze, mpeti­peti na msifie! Ukiikamilisha kwa ukamilifu hatua hii ya kwanza na ya muhimu, basi utakuwa tayari umeshamuingiza kwenye safari ya kuelekea kufurahia tendo.

Mnapokuwa eneo la tukio, hu­takiwi kuwa na papara! Lazima kwanza na wewe akili yako uitu­lize na badala ya kukimbilia ku­ingia mchezoni na kuanza kupiga mbizi kama mtu anayejifunza kuogelea, unatakiwa kwanza ku­tumia muda wa kutosha kupasha misuli moto.

Muda unaoshauriwa kitaala­mu, ni angalau dakika thelathini

 

ndani ya muda huu mfanyie yale mambo yatakayoamsha hisia zake za ndani, viungo vya mwili wako kama mikono, vi­dole, mdomo, masikio vinaweza kuzalisha hisia nzuri sana kama utakuwa unajua nini unatakiwa kufanya kwa wakati gani.

 

Narudia tena, epuka kuwa na papara za kukimbilia uwanjani, maandalizi ni muhimu sana kwani yatamuandaa mwenzi wako kimwili na kihisia. Ukiwa na uhakika kwamba maandal­izi yamefanyika kwa ukamilifu, sasa unaruhusiwa kuendelea na hatua kubwa na ya muhimu inayofuatia.

 

Katika hatua hii ambayo kimsingi ndiyo inayowaungani­sha, pia unatakiwa kuwa na uelewa juu ya nini cha kufanya na kwa mtindo gani, siyo un­aingia kwa papara kama un­akimbizwa, hapana. Hapa pia unatakiwa kujifunza zaidi ili kuhakikisha unaibuka mshindi kwa kumfikisha mwenzi wako kwenye kilele cha safari yake ya huba.

Kwa leo tuishie hapa, tutaen­delea wiki ijayo sehemu ya pili.

Facebook: Hash Power
Insta: Hashpower 7113
WhatsApp: 0719 401 968

Comments are closed.