The House of Favourite Newspapers

Mbinu za Pluijm, Mayanja zafanana

0

PLUIJMKITAMBIKocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm.

Waandishi Wetu, Dar es Salaam
MBIO za ubingwa wa Ligi Kuu Bara zimekolea, ushindani sasa unaanza kuonekana kuwepo kwa timu tatu za juu ambazo ni Yanga, Azam na Simba, lakini wakati presha ikiwa kubwa pande zote, imebainika kuwa hata mbinu za mazoezi baina ya timu hizo zimekuwa hazitofautiani kwa kiwango cha juu.

tafiti uliofanywa na gazeti hili umebaini mbinu za Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm na yule wa Simba, Jackson Mayanja, zinafanana kiasi kwamba unaweza kuhisi ni kama wanaibiana mbinu za kusaka mabao kwa jinsi wanavyowafundisha wachezaji wao siku za hivi karibuni.

Yanga inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, huku Simba nayo ikijiandaa kuwavaa African Sports katika Uwanja wa Taifa, Dar ambapo michezo hiyo yote inatarajiwa kupigwa kesho Jumamosi.

Katika mazoezi ya Jumanne wiki hii waliyofanya Simba kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Dar, Mayanja, raia wa Uganda, alikuwa akiwanoa mastraika wake jinsi ya kufunga mabao ya mbali na karibu katika mazingira tofauti.

Washambuliaji wa Simba waliokuwa wakifanyishwa mazoezi hayo ni Hamis Kiiza, Joseph Kimwaga, Hija Ugando na Ibrahim Ajib huku Paul Kiongera na Danny Lyanga wakiwa hawapo.

Washambuliaji hao walikuwa wakitengewa mipira katika ‘engo’ ya pembeni nje ya eneo la hatari na kutakiwa kupiga mashuti kisha wakawa wanabadilishiwa sehemu kwa kuwekewa karibu na lango na kutakiwa kufanya hivyo.

Kuzuia mashuti hayo, Simba iliwatumia makipa wake wote ambao ni Peter Manyika, Vincent Angban, Khomeni Baruani na David Kisu ambapo walikuwa wakipokezana.
Siku moja baada ya Simba kufanya mazoezi hayo, Pluijm naye akawa anawanoa wachezaji wake jinsi ya kufunga mabao kwa ‘engo’ zote huku wachezaji hao wakionekana kuelewa zoezi hilo.

Alichofanya Pluijm ni kutumia nusu uwanja kisha wachezaji wakawa wanacheza pamoja lakini akiwataka anayepata nafasi apige shuti kali langoni.

Zoezi hilo likawa endelevu ambapo kiungo Thabani Kamusoko ndiye alionekana kupatia kwa mashuti yake mengi kulenga lango huku straika Paul Nonga akikosea mara kadhaa.

Leave A Reply