
Kampuni ya uchimbaji wa madini Tanzania – Acacia inatarajia kuzindua mashindani ya mbio za baiskeli kwa lengo la kukusanya zaidi ya Sh milioni 340 kzitakazotumika kuboresha upatikanaji wa elimu kwa jamii zinazozunguka migodi yetu katika kanda ya ziwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini, Asa Mwaipopo, Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben alisema mashindano hayo wameyapatia jina la ‘Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge’.
Alisema masindano hayo yatazinduliwa rasmi Oktoba 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo na mashindano yenyewe yataanza Novemba 3 mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Pia alisema mashindano hayo yanaenda sambamba na mpango wa kampuni wa kujenga jamii endelevu.
Alisema mpango huo unaofahamika kwa jina la ‘CanEducate’,unatoa kipaumbele katika kuhakikisha watoto wa kike – wanapata elimu bora kama njia moja wapo ya kujikwamua na umaskini.
“Fedha hizo zitasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia maskini na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia sare na vifaa vingine vya shule ikiwemo vitabu na vifaa mbalimbali,” alisema.
Alisema hadi sasa mpango huo wa CanEducate ulioanza mwaka 2011, umetumia kiasi cha Sh milioni 494 kwa kuwadhamini wanafunzi 3936, na kuziwezesha kwa njia mbalimbali shule zaidi ya tisa.
“Tunatoa wito kwa kampuni na wadau mbalimbali kujitokeza katika kuchangia kufikia lengo letu ili kwa pamoja tuweze kuleta tumaini la thamani kwa wanafunzi wenye ndoto ya kupata elimu nzuri na kufikia malengo yao, na baadae kuja kulisaidia taifa.
Naye Rais wa Chama cha Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama alitoa wito kwa wananchi na makampuni mbalimbali kujitokeza katika mbio hizo na kufadhili mpango huo ili kuiwezesha jamii kupata huduma mbalimbali za kielimu.
Aidha, baadhi ya wanufaika wa mpango wa CanEducate, Dk. Husein Mwanga ambaye ni mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili, alisema mpango wa CanEducate ulimwezesha kusoma shahada ya uzamivu katika masuala ya usalama kazini.
Naye Dismas Kalitenge alisema licha ya mpango huo kumwezesha kulipia baadhi ya gharama katika Shahada ya Uhandisi wa madini aliohitimu mwaka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia sasa amepata ufadhili wa msomo ya Shahada ya Uzamivu nchini Canada.
NA MWANDISHI WETU


Comments are closed.