The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mbivu Mbichi Bifu Zito Chuchu vs Tessy

0

DAR: Lile bifu zito la waigizaji wa Bongo Movies; Chuchu Hans na Tessy Abdul ‘Tessy Chocolate’ bado linafurukuta, IJUMAA lina mbivu na mbichi juu ya sakata hilo.

 

Chanzo cha habari kimeliambia IJUMAA kuwa, hivi karibuni wawili hao walitaka kuzichapa kavukavu wakiwa lokesheni wakishuti tamthiliya mpya ya Slay Queens.

 

Tessy ambaye awali alijulikana kama mrembo maarufu wa mitandaoni (sosholaiti) kabla ya kujiingiza kwenye Bongo Movies, amepata nafasi ya kuigiza kwenye tamthiliya hiyo.

 

SABABU YA BIFU

Mwanzo ilisemekana kwamba, Tessy na Chuchu walikuwa na ushosti na Chuchu ndiye aliyemtafutia Tessy nafasi ya kucheza tamthiliya hiyo.

 

Gazeti la IJUMAA linafahamu kuwa, sababu kubwa ya bifu hilo ni kile kitendo cha Tessy kutuhumiwa kutoka kimapenzi na mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye ni mzazi mwenza wa Chuchu.

 

Baada ya kupata habari hizo, IJUMAA liliwatafuta wahusika ili kuzungumzia ugomvi wao ambapo kila mmoja alijibu lake kwa wakati wake.

 

CHUCHU SASA

Kwa upande wa mwanamama Chuchu, alipoulizwa kuhusiana na bifu hilo ambalo linaendelea kati yake na Tessy, alijibu kuwa, hawezi kumzungumzia Tessy, kwani ni sawa na kumpa jina (umaarufu).

 

“Siwezi kuliongelea hilo kwa sababu kumuongelea huyo mtu, ni sawa na kumpa umaarufu kwa watu kwa sababu yangu,’’ alisema Chuchu.

 

TESSY NAYE

Alipotafutwa Tessy ili kuzungumzia ishu hiyo, alidai hana ukaribu na mwanamama Chuchu.

“Mimi na Chuchu hatujawahi kuwa na ukaribu wowote, hivyo siwezi kumuongelea kwani hata kupata nafasi ya kuigiza, ni watu wengine kabisa waliniunganisha na wala si yeye,’’ alisema Tessy na kukata simu.

 

Kwa muda mrefu tangu Tessy alipotuhumiwa kutoka kimapenzi na Ray, wawili hao wamekuwa hawaivani kwenye chungu kimoja.

Stori: HAPPYNESS MASUNGA, Ijumaa

Leave A Reply