The House of Favourite Newspapers

Mbivu na Mbichi Kujulikana leo katika Uwanja wa Emirates, Arsenal vs Man United

0

MBIVU na mbichi zitajulikana leo katika Uwanja wa Emirates ambao kwa sasa mashabiki wa Arsenal wanauita jehanamu ya soka kutokana na vipigo ambavyo wamekuwa wakitoa kwa wapinzani msimu huu.

Hapa unazungumziwa mchezo wa Premier kati ya Arsenal na Manchester United ambao utapigwa leo Jumapili katika Dimba la Emirates.

Utakuwa ni mchezo wa kipekee na wa aina yake,hii ni kutokana na ubora wa timu husika ambazo zinaenda kukutana hasa Arsenal ambao kwa msimu huu wamekuwa sio wa kubeza wakiongozwa na nahodha wao, Martin Odegaard.

Arsenal itakuwa nyumbani Emirates ikisaka ushindi na ikipambana kulipa kisasi kwa Man United baada ya kuambulia kipigo pale Old Trafford cha mabao 3-1, mechi ya kwanza.

Hakika hautakuwa mchezo rahisi hata kidogo hasa kwa upande wa Man United na hii kutokana na ubora wa Arsenal katika maeneo yote.

Arsenal wamekuwa imara katika maeneo yote kuanzia kupachika mabao hadi kuzuia jambo ambalo linawapa nafasi zaidi ya kupata matokeo bora katika mchezo huu na hasa wakiwa mbele ya mashabiki wao pale Emirates.

Wakati Bukayo Saka, Odegaard wakiwa tishio, upande wa pili Marcus Rashford ni kama amezaliwa upya na ndiye mchezaji wa safu ya ushambuliaji ambaye anaangaliwa zaidi pale United.

Hivyo Man United wanatakiwa kucheza kwa akili na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, ukiangalia katika mchezo wa leo wanamkosa kiungo wao muhimu, Casemiro, ambaye amepata kadi ya njano katika mchezo uliopita na kumfanya kutumikia adhabu.

Kiungo huyo amekuwa chachu ya mafanikio kwa United katika eneo la kiungo, hivyo kukosekana kwake kutakuwa ni pengo kubwa.

Ukiangalia uimara wa mabeki wa Arsenal ukiongozwa na William Saliba, Gabriel na Ben White, umekuwa sio wa kubeza hasa katika kuruhusu mabao na safu ya ulinzi ya Arsenal ipo imara huwezi kufananisha na ile ya Man United ingawa kucheza kwa Luke Shaw kama beki wa kati sambamba na Raphael Varane, wamekuwa wakifanya kazi kubwa japo kuna makosa madogomadogo.

Hivyo kazi haitakuwa rahisi ndani ya Emirates na mchezo wa leo ndiyo utaonyesha picha halisi kama Man United walibahatisha kuifunga Arsenal au United watakuwa baba lao tena.

Hii ni kutokana na na kwamba katika msimu wa 2022/23 tangu umeanza Arsenal imepoteza mechi moja pekee kabla ya mchezo wa leo na mchezo huo ulikuwa ni dhidi ya Man United, sasa mbivu na mbichi ndiyo zitajulikana hapa.

Ikumbukwe katika vita ya leo, Arsenal yeye atakuwa anaendelea kupambana kukusanya pointi za kuwania ubingwa msimu huu, lakini Man United baada ya kupunguzwa kasi na Crystal Palace itakuwa inapambania nafasi yake kuhakikisha inasalia ndani ya top four bila kupinduliwa na Tottenham.

Kwa hiyo Arsenal na Man United kila mmoja anatinga kwenye mchezo huu akiwa na malengo yake hasa ya kuhakikisha anasaka pointi tatu muhimu.

Lakini vita hii itaendelea kuonesha ubora wa Kocha Mikel Arteta ambaye kwa sasa ameibadili Arsenal na kuwa timu tishio ndani ya Premier League, huku Erik ten Hag na yeye anapambana kujaribu kuirudisha Man United kwenye ramani ya soka baada ya kupotea kwa muda mrefu.

VIKOSI

ARSENAL; Ramsdale, White, Gabriel, Saliba, Zinchenko, Martinelli, Xhaka, Partey, Saka, Odegaard, Nketiah.

MAN U; De Gea, Varane, Shaw, Wan-Bissaka, Malacia, Fernandes, Fred, McTominay,Eriksen, Rashford, Martial.

MATOKEO YA MWISHO PREMIER

Man United     3-1   Arsenal

Arsenal              3-1   Man United

Man United     3-2   Arsenal

Arsenal              0-0   Man United

Man United     0-1   Arsenal

Arsenal              2-0   Man United

Man United     1-1   Arsenal

Arsenal              2-0   Man United

Man United     2-2   Arsenal

Man United     2-1   Arsenal

ALI KAMWE AMCHAMBUA MAMADOU, ISHU ya FEISAL “TUTAZUNGUMZA KESHO”

Leave A Reply