The House of Favourite Newspapers

Mbivu na Mbichi Makundi UEFA leo, Vigogo Kumi Kikaangoni Matumizi Mabaya ya Fedha

0
Ratiba ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

LEO Agosti 25, 2022 katika jiji la Istanbul huko Uturuki yatapangwa makundi ya timu zilizofuzu kushiriki hatua ya makundi ya klabu bingwa Ulaya pamoja na kufanyika kwa mkutano wa kwanza msimu huu wa bodi ya shirikisho la klabu za Ulaya.

 

Majira ya saa 1 usiku saa za Afrika mashariki itafanyika droo kwa timu zilifuzu kushiriki hatua ya makundi klabu bingwa ulaya huku vigogo mbalimbali kama Liverpool na Chelsea wakiomba kuepuka kupangwa kwenye makundi magumu ili wapate muda wa kutosha kurudisha ubora wao baada ya mwanzo usio wa kuridhisha wa msimu.

Rais wa PSG Nasser Al-Khelaïfi

Kwa upande mwengine bodi ya shirikisho la klabu za Ulaya ikiongozwa na Nasser Al-Khelaïfi ambaye pia ni rais wa klabu ya PSG, itafanya mkutano leo utakaokuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo kuzizungumzia klabu kumi za ulaya PSG ikiwemo zilizokiuka kanuni ya ‘Financial Fair Play’ kwa kufanya matumizi kupitiliza kinyume cha kanuni za shirikisho hilo.

 

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply