The House of Favourite Newspapers

Mbona Hatukamati Fursa? Why?

0
Successful businesspeople raising hands upward.
Successful businesspeople raising hands upward.

Kiukweli sijui sisi Wabongo kwa nini hatutawali dunia, kila kitu tunachosema nia ndio hatuna. Siku nyingine nikifikiria inaniboa sana. Kwa nini hawa Wachina na Wamarikani waonekane ndio wajanja wakati hali halisi sisi ndio tuna kila kitu?

Yaani sisi wagumu sana kutumia fursa, hii ndio inayochelewesha ndoto yangu ya kutawala dunia. We fikiria tangu napata akili za kuuelewa ulimwengu, nimekuwa nikisikia habari na matangazo kuwa kuna watu wanaweza kufanya chochote kile. Ukiwaendea wanaweza kukupa utajiri, usiku wanapaa hawana haja ya ndege wala nini, ungo tu unasaidia kufika popote pale.

Yaani kimsingi wanaweza kufanya chochote. Ukiangalia hata jamaa umkute mjanja mjanja vipi, ukifuatilia lazima aende kwa watu hawa ili asaidiwe kufanikiwa mambo yake. Nasikia ukiwa na timu ya mpira unataka kuwafunga wenzio, unawaendea hawa jamaa wanafanya mambo yao lazima timu yako iwafunge wapinzani.

Ukitaka uongozi we waambie tu hawa jamaa wanafanya mambo unapata cheo. Hata shuleni huna haja ya kusoma, we unawaona hawa jamaa ukifika chumba cha mtihani majibu unayaona yamekwisha andikwa.

Juzi kabinti fulani kamesema kanatafuta kipaji cha kuongea Kiingereza, mi nakashangaa, si kangeenda kuwaona hawa jamaa kesho yake tu kangekuwa kanaongea Kiingereza kama vile kamezaliwa London.

Hawa wataalam wanajulikana kuwa wanaweza kufanya mtu asahau deni, kwa nini serikali haiwatumii hawa ili kusahaulisha deni la Taifa, jamaa wakiamka asubuhi wenyewe wanatuandikia barua kuwa hatuna deni nao. Kwa kuwa hawa jamaa ni mabingwa wa kutoa dawa za mvuto, yaani mtu anaanza kukupenda tu, sasa hii dawa tungewaroga Wamerikani waanze kutupenda tu wenyewe waanze kulilia rais wetu awatawale na wao.

Yaani ukiangalia fursa kibao. Serikali ingeweza hata kuwaita hawa jamaa wakafanya mambo yao wale wote walioficha sukari tukawaona wenyewe wamebeba viroba vya sukari wanarudisha vituo mbalimbali vya polisi.

Leave A Reply