The House of Favourite Newspapers

Mbosso Aingia Woga Kumshauri Diamond!

SEPTEMBA 21, 2014 yawezekana ikawa ni siku muhimu ya kumbukumbu kwa staa wa Bongo Fleva, Mbwana Yussuph Kilungi ‘Maromboso’ kwani alikuwa akitambulishwa rasmi akiwa na Kundi la Yamoto Band ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Hata hivyo, Yamoto Band haikudumu sana, ikasambaratika huku kila mmoja akifanya kazi kivyake.

 

Kusambaratika kwa kundi hilo kukatengeneza historia nyingine kwa Maromboso ambapo Januari 28, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar alitambulishwa rasmi kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Diamond Platnumz.

Kutambulishwa kwake kukazaa jina jipya la Mbosso Khan au Mbosso. Tangu aingie rasmi WCB amefanikiwa kutoa nyimbo nyingi mfululizo kama vile Watakubali, Alelee, Nimekuzoea, Picha Yake na Nadekezwa.

 

Huyu ndiyo Mbosso ninayemfahamu! Risasi Vibes limefanikiwa kufanya naye ‘Exclusive Interview’ juu ya maisha yake na muziki kwa ujumla, huyu hapa anatoa majibu mafupi lakini ya kueleweka;

Risasi Vibes: Role model wako ni nani katika muziki?

Mbosso: Mmh!Sina Role Model.

Risasi Vibes: Umeanza kujihusisha na muziki ukiwa na umri gani?

 

Mbosso: Kati ya miaka 19 au 18.

Risasi Vibes: Familia yako hawakuleta shida yoyote waliposikia unajihusisha na muziki?

Mbosso: Walileta shida sana ila baadaye wakabariki.

Risasi Vibes: Ulijisikiaje Diamond alipokutangaza rasmi kuwemo WCB?

Mbosso: Nilifurahi sana.

Risasi Vibes: Unapenda sana kutaja neno Kibiti kwenye nyimbo zako, ni kwenu au?

Mbosso: Kibiti ndio sehemu niliyotokea.

Risasi Vibes: Nani aliyekushawishi kujiunga WCB?

Mbosso: Hakuna mtu aliyenishawishi.

Risasi Vibes: Ulishawahi kujuta kujiunga WCB?

Mbosso: Hapana sijawahi.

Risasi Vibes: Tutegemee lini ngoma mpya?

Mbosso: Soon! (hivi karibuni).

Risasi Vibes: Mwanzo ulikuwa Yamoto Band, ni nani ambaye alikuwezesha kujiunga hapo?

 

Mbosso: Nilifanyiwa interview kwa sababu mwanzo nilikua Mkubwa na Wanawe.

Risasi Vibes: Ulijisikiaje Yamoto Band ilipovunjika?

Mbosso: Niliumia sana na ilinichukua muda kusahau.

Risasi Vibes: Ulikuwa unafanya nini baada ya kundi hilo kuvunjika maana ulikuwa kimya sana?

Mbosso: Nilikua nafikiria sehemu sahihi ambayo naweza nikafanya kazi.

Risasi Vibes: Ushawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Queen Darleen?

Mbosso: Hapana sijawahi.

 

Risasi Vibes: Upo katika uhusiano na Rukia ‘Rucky Baby’ (mpenzi wa zamani wa Rayvanny)?

Mbosso: (anacheka) Hapana!

Risasi Vibes: Wimbo gani ambao uliuimba ukiwa Yamoto Band na hadi leo ukiusikia unakusisimua?

Mbosso: Nyimbo zote.

Risasi Vibes: Mara yako ya mwisho kukataliwa na mwanamke ni lini?

Mbosso: Aaaaah! Sikumbuki ila ni zamani sana.

 

Risasi Vibes: Kwa nini Mbosso WCB? Sio Aslay, Enock Bella wala Becka Flavour?

Mbosso: Nafikiri swali hilo linawafaa viongozi wangu (Diamond).

Risasi Vibes: Skendo za Diamond zinakuathiri vipi wewe kama mwanafamilia wa WCB?

Mbosso: Haziniathiri hata kidogo.

Risasi Vibes: Ushawahi kumshauri Diamond kuhusu uhusiano wake?

Mbosso: (anakaa kimya kidogo) Kuna mambo ya kumshauri lakini sio mapenzi.

 

Risasi Vibes: Una mtoto au watoto?

Mbosso: Nina watoto wawili.

Risasi Vibes: Una ndoto ya kuwa na msichana wa aina gani?

Mbosso: Anayeijua dini na ambaye ameshamaliza ujana.

Risasi Vibes: Ukisikia ‘NO COMMENT’ unaelewa nini?

Mbosso: (anacheka) ninavyoelewa mimi ni kwamba hamna kitu chochote cha kujibu.

 

Risasi Vibes: Umefanikiwa kusoma hadi kidato cha ngapi?

Mbosso: Kidato cha nne.

Risasi Vibes: Ni kweli unashindana na Aslay kimuziki?

Mbosso: Hapana, mimi nafanya muziki wangu.

Risasi Vibes: Unaweza kufanya kolabo na Alikiba?

Mbosso: Ishu ni menejimenti tu, wakikaa chini wakizungumza mimi sina tatizo si biashara?

Risasi Vibes: Wimbo gani wa Alikiba unaupenda na unajua kuuimba?

 

Mbosso: Unaitwa Hadithi, naupenda sana.

Risasi Vibes: Ukifukuzwa sasa hivi WCB utaenda kwenye lebo nyingine au utajisimamia mwenyewe?

Mbosso: (anacheka) Daah! Nitarudi kujisimamia mwenyewe.

Risasi Vibes: Kati ya mama, mke na mtoto ni yupi ambaye ana umuhimu sana kwako?

Mbosso: Mama ni muhimu sana kwangu.

Risasi Vibes: Ni kitu gani cha muhimu huwezi kukiacha ukiwa unaenda kushoot video ya wimbo?

 

Mbosso: Nguo.

Risasi Vibes: Mbali na muziki ni kitu gani kingine unafanya ili kujiingizia kipato?

Mbosso: Kuna vitu ambavyo navifanya ila siwezi kuweka wazi kwa sasa.

Risasi Vibes: Unajiona wapi baada ya miaka mitano?

Mbosso: Najiona mbali sana, yaani najiona Mbosso wa kimataifa.

 

Shamuma Awadhi

FUATILIA SIMULIZI YA MAISHA YA ALIKIBA HAPA

Comments are closed.