The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mbosso Amwagana na ‘Mkewe’, Amkumbuka Marehemu Martha

0

 

HABARI zinazosambaa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii zinadai kwamba msanii wa Bongo Fleva, Mbosso,  ameachana na mzazi mwenzake aitwaye Rukia ambaye miezi michache iliyopita walibahatika kupata mtoto.

 

Kwa mujibu wa watu wake wa karibu, inasemekena wawili hao wametibuana vibaya na kila mmoja kuamua kuendelea na maisha yake huku chanzo kikiwa hakijajulikana. Inadaiwa kuwa bidada huyo ni mwanamke wa nne kuachana na Mbosso.

Baada ya hayo kutokea, kupitia ‘Account‘ yake ya SnapChat, Mbosso aweka picha ya marehemu mpenzi wake ambaye alikuwa muigizaji maarufu nchini, Boss Martha,  na kuandika ujumbe ambao umeashiria simanzi yake; “Lini nitakuona tena” na kuweka ‘Emoji‘ yenye ishara ya maumivu.

Staa wa muziki nchini ambaye ni bosi wa Mbosso, Diamond Platnumz , na Romy Jones wamempa faraja na kumwambia awe ni mwenye subira katika hili.

Martha alifariki dunia Septemba 11, 202o, ambapo wawili hao walidaiwa kuzaa mtoto licha ya kuficha mahusiano yao huku Mbosso akidai kunyimwa mtoto aliyedai wake huku ndugu wa marehemu wakisema kuwa marehemu hakuwaeleza kama alizaa na Mbosso.

 

Leave A Reply