Mbosso Atoboa Siri ya Kubaki WCB

WAKATI memba mwenzao wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Harmonize akidaiwa kuondoka lebo hiyo, mkali wa Bongo Fleva, Mbosso ametoboa siri ya yeye kubaki.

 

Akipiga stori mbili tatu na Showbiz, Mbosso alisema kitu kinachomfanya aendelee kuithamini na kubaki katika lebo hiyo ni kitendo cha kumchukua kipindi kukiwa hakuna mtu aliyemhitaji.

 

“Watu hawaelewi tu, ngoja niwape siri! Katika kipindi ambacho WCB inanichukua, kulikuwa hakuna mtu anayenihitaji yaani hakuna mtu aliyekuwa anaamini ndani ya Mbosso, WCB ikanichukua na kufanya asilimia kubwa ya watu kuniamini,” alisema Mbosso.


Loading...

Toa comment