The House of Favourite Newspapers

Mbosso Khan Asema Anatamani Kuwa na Wapenzi Wanne

0
Mbosso msanii wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi

MBOSSO Khan; ni mwimbaji mkali wa Tanzania ambaye amefunguka kuhusu jinsi angefurahi kuwa na wapenzi wanne. Mbosso amesema; “Ukiwa na mpenzi mmoja anakupa furaha.

Imagine ukiwa na wapenzi wanne hayo mafuraha yake…” Si mara ya kwanza kwa Mbosso kuzungumza kuhusu kuwa na wapenzi wengi.

Mwaka 2020, Mbosso anayetumikia Lebo ya WCB alisema kuwa wake wanne hawatoshi, angependelea kuwa na wanawake 15 hadi 20.

Mbosso amesema anatamani kuoa wapenzi wanne

“Lakini kwangu, wanawake wanne ni wachache sana,” alisema Mbosso alipohudhuria harusi ya Esma Platnumz; dada wa Diamond Platnumz. Mbosso ni Muislam na anaruhusiwa kuoa wake wanne.

Jumuiya za Kiislam zinaruhusu hadi wake wanne. Mbosso tayari ni baba wa watoto watatu kutoka kwa wanawake tofauti.

Leave A Reply