Mbosso: Krismasi Hii Dar Live Hapatoshi!

MKALI anayekimbiza kwenye Bongo Fleva akitokea Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mbwana Yusuf Kilungi ‘Mbosso Khan’, amefungukia shoo yake atakayoifanya Sikukuu ya Krismasi ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, kuwa itakuwa hapatoshi.

 

Mbosso ameiambia Ijumaa Showbiz kuwa, siku hiyo ya (Desemba 25) atapiga shoo baab’kubwa kwani ni muda mrefu umepita hajafanya shoo Mbagala hivyo ana shauku mno kwani huko ndiko nyumbani kwao.

 

“Nimejipanga vizuri, nina mazoezi ya kutosha hivyo watu wangu wa Mbagala wategemee kitu kikubwa na ninaahidi sitawaangusha.

 

“Siku hiyo ndiyo watajua kama kweli ninaitwa Mbosso kwani nimewaandalia madude ya kutosha ambayo naamini watayafurahia, hapa ninavyoongea na wewe nimetoka kumaliza mazoezi na madansa wangu na wao wanaahidi kitu kizuri. Mbagala wakae mkao wa kula,” alisema Mbosso.

AMMAR MASIMBA

 

 

Toa comment