The House of Favourite Newspapers

MBOWE Alivyoitwa Mbele ya Makamu wa Rais “Yuko wapi?” – VIDEO

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu amehitimisha ziara yake katika mkoa wa Kilimanjaro katika Wilaya ya Hai na kuzungumza na umati wa wananchi waliojitokeza kumsikiliza.

 

Katika Ziara hiyo aliongozana na Mawaziri wawili, waziri wa Tamisemi Selemani Jafo na Wilium Lukuvi.

 

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu alidai kutamani sana kusikiliza changamoto za wakazi wa Hai kutoka kwa mwakilishi wa wananchi ambaye ni Mbunge wao ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe lakini hakuwepo katika mkutano huo.

 

“Nilitamani mbunge wenu awe hapa atueleze mafanikio na changamoto zenu lakini hayupo, “ alisema Samia.

VIDEO: MSIKIE SAMIA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.