The House of Favourite Newspapers

MBOWE ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI

IKIWA ni takribani saa 24 tangu alazwe katika Hospitali ya Taifa Kitenngo cha Dharula, Afya ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe imeimarika na ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo huku akieleza kuwa kilichokuwa kikimsumbua ni msongo wa mawazo na uchovu kupita kiasi.

 

Mbowe ameeleza hayo leo Jumanne, Juni 19, 2018 wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari waliofika Muhimbili na kusema kwa sasa afya yake ni mzima, baada ya kumaliza msiba ataendelea kufanya vipimo  maalumu vya kiafya kwa kadiri ambavyo atatakiwa na madaktari wake kama itakuwa ndani au nje ya nchi.

 

Mbunge huyo wa Hai, amewashukuru viongozi wa vyama mbalimbali na Watanzania ambao walimtembelea na waliokuwa wakimuombea kwa njia mbalimbali katika kipindi hiki yeye na familia yake, pia waliozuiwa kumuona kutokana na sheria za kitabibu.

Comments are closed.