The House of Favourite Newspapers

MBOWE ATANGAZA MGOMO MPYA BUNGENI – VIDEO

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ametangaza mgomo mpya kwa wabunge wa upinzani akisema hawatasoma maoni yao kuhusu bajeti ya serikali ya mwaka 2018/2019 kwa wizara zote mpaka pale malalamiko yao yatakapofanyiwa kazi.

 

Mbowe amesema hayo jana, Jumatano Aprili 4, 2018 mjini Dodoma na kueleza kuwa wamefikia uamuzi huo kwa sababu watumishi wa Ofisi ya upinzani ambao ndiyo huwasaidia kuchapa ripoti, kuandika hotuba na kufanya tafiti mbalimbali kuondolewa bungeni. Ameeleza kuwa kuondolewa kwa watumishi hao ni kinyume cha kanuni za Bunge huku akidai, kwa mujibu wa sheria za bunge, ofisi ya upinzani lazima iwe na watumishi, kuwanyima haki zao bungeni.

 

Aidha, Mbowe amesema yeye kama mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzania bungeni, amenyimwa gari na dereva tangu Januari mwaka huu, jambo ambalo amedai ni kunyimwa haki yake.

“Sina gari la serikali wala dereva, nilinyang’anywa tangu Januari natembelea gari binafsi kwa sasa, licha ya kuwa ni haki yangu. Sijililii mwenyewe, ninayo magari mengi nitatumia na hata nikikosa wabunge hapa watanipa gari la kutembelea,” alisema Mbowe.

 

TAZAMA VIDEO MBOWE AKIFUNGUKA

 

Comments are closed.