The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yalizuia Jeshi la Polisi Kumkamata Mbowe

Mbowe na makada wengine wa Chadema wakitoka mahakamani

Mbowe akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama.

 

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, leo amefika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kufuatilia mwenendo wa kesi ya kikatiba aliyoifungua dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Camilius Wambura.

Katika kesi hiyo,  mbali na mambo mengine, Mbowe anapinga amri ya Makonda ya kutaka akamatwe na pia kile alichokiita kudhalilisha watu wakati mkuu huyo wa mkoa alipotaja majina ya watu.

Kesi imeendelea kunguruma na ilibidi iahirishwe mpaka saa saba mchana ambapo walipoingia mahakamani kwa mara nyingine,

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imetupilia mbali ombi la Jeshi la Polisi la kutaka kumkamata M/kiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kukubali maombi ya mawakili wa Mbowe kwamba asikamatwe hadi tarehe Februari 23, mwaka huu kesi itakaposikilizwa tena.

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imelizuia Jeshi la Polisi kumkamata Freeman Mbowe hadi Feb. 23 maombi yake yatakaposikilizwa huku ikieleza kuwa Jeshi hilo linaweza kumuita Freeman Mbowe kwa mahojiano kama litaona umuhimu wa kufanya hivyo, lakini hawaruhusiwi kumkamata.

Comments are closed.