The House of Favourite Newspapers

Mbowe: Mashtaka Yetu ni ya Kisiasa – Video

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mashtaka yanayowakabili ni mashtaka ya kisiasa, yanayoficha waliokosa na kuwahukumu waliokosewa.

 

Amedai kuwa kwa ujumla mashtaka hayo yanayowakabili siyo ya kweli. Mbowe ambaye alianza kujitetea Novemba 4 na 5 mwaka huu, aliyaeleza haya Novemba leo Novemaba 8 mwaka huu wakati akiendelea kutoa utetezi wake huku akiongozwa na Wakili, Peter Kibatala Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

 

Katika Kesi hiyo Mbowe na wenzake 8 wanaokabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.

 

Pia wanadaiwa kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi makosa yanayodaiwa kutendeka kati ya Februari 1 na 16, 2018, jijini Dar es Salaam.

 

Mbali na Mbowe wengine Wanaokabiliwa katika kesi hiyo, mbali naMwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

 

Wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Comments are closed.