The House of Favourite Newspapers

Mbowe mgeni rasmi siku ya vijana duniani, waanza na usafi Mwanza

0

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe.Freeman Mbowe anatarajia kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya vijana Duniani yaliyoandaliwa na Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) katika Uwanja wa Furaisha Jijini hapa.

Hayo yameelezwa na Katibu wa baraza la vijana la chama hicho (Bavicha) Mkoa wa Mwanza Ester Fulano wakati wakifanya usafi katika soko la Mbugani katikati ya Jiji la Mwanza kama Hamasa ya kuelekea kwenye kongamano hilo linalotarajiwa Agosti 12 Mwaka Huu.

Fulano amesema pamoja na mambo mengine Kongamano hilo pia litaweza kujadili mambo mbalimbali dhidi ya nchi hususani vijana na umachinga,ukosefu wa mitaji, wafungwa gerezani kwa masuala ya kisiasa.

Kwa upande wake Michael Christian mwenyekiti wa (BAVICHA) wilaya ya nyamagana, amewapa hamasa wananchi katika suala la usafi kwani usafi ni afya  lakini pia kuwakumbumbusha watu majumumu yao ya kisiasa na kijamii na lengo kubwa likiwa ni makaribisho ya siku ya kongamano la vijana duniani.

“ijue na itumie nguvu yako” hii ni kauli mbiu ya  kongamano hilo ikiwa inalenga kutoa fursa kwa vijana kujitambua na kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwenye taifa lao ikiwa ni pamoja na kuunganisha sauti kwa pamoja bila kujali chama na  hali ambayo itoa viongozi wazuri wenye kuwajibika katika taifa lao.

 

Na TRINY GOODLUCK- GPL

Leave A Reply