Mbowe, Matiko Wafutiwa Dhamana, Sasa Rumande Hadi Kesi Imalizike – Video

Mahakama ya Kisutu, imewafutia dhamana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana, kuanzia sasa watarudishwa rumande hadi kesi yao itakapomalizika.

Uamuzi huo unatokana na maombi yaliyotolewa na upande wa mashtaka Novemba 12, uliodai washtakiwa hao wamekiuka masharti ya dhamana kwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama na kushindwa kuripoti katika kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala.

Upande wa mashtaka ulifikia hatua hiyo baada ya Mbowe kushindwa kufika mahakamani, Novemba Mosi na 8 na Matiko kushindwa kufika Novemba 8, kwa ajili ya usikilizwaji wa awali wa kesi inayowakabili.

Mbowe, Matiko na wenzao saba wanakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani hapo yenye jumla ya mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi na uchochezi wa uasi.

BREAKING: MBOWE Afutiwa Dhamana,Arudishwa Rumande

Toa comment