The House of Favourite Newspapers

Mbowe na Wenzake Wapewa Siku 14 Kuanza Kujitetea

LEO Jumatatu, Oktoba 21, 2019, viongozi 9 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wameshindwa kuanza kutoa utetezi wao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kuomba kupewa muda wa kujiandaa.

 

Awali upande wa utetezi uliomba kupewa wiki 3 za kujiandaa lakini Hakimu mkazi Simba ametoa uamuzi wa kuwapa wiki mbili tu za kujiandaa kwa ajili ya utetezi wao kabla ya ushahidi kutolewa.

 

Hatua hii imefikiwa baada wakili wa Utetezi Peter Kibatala kuomba wateja wake wapewe wiki tatu za kujiandaa mnano October 18. Viongozi hao wanatarajiwa kuanza kujitete kwa siku tatu mfululizo, kuanzia Novemba 4, 5 na 8 mwaka huu.

 

Leo Upande wa utetezi ulitakiwa kuanza kutoa utetezi wao katika kesi hiyo baada ya maombi yao ya mashahidi kusikilizwa kabla yao kutupiliwa mbali Octoba 15.

Hakimu Mkazi Thomas Simba ameahirisha Kesi hiyo hadi Novemba 4 mwaka huu ambapo washitakiwa wataanza kutoa utetezi wao.

 

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama ya kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki kushawishi hali ya kutoridhika na uchochezi kati ya Februari 1 na 16, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.